HEBU msomaji cheki jinsi wenzetu wa Ulaya wanavyofanya mambo yao ya kiufundi kistaili!

Ijumaa, 9 Agosti 2013

DUDU BAYA MBARONI KWA KUCHOMA MOTO NYUMBA YA GEEZ MABOV MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameswekwa rumande kwa kudaiwa kuchoma nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez Mabovu’, Mashaka Mrisho. Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo mwenye nyumba sambamba na polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa madai ya kuchoma moto nyumba kwa makusudi na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay. “Mkewe alitupia mkaa wa moto katika sofa, likashika moto kabla majirani hawajanisaidia kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha ndipo nikawapeleka polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja kumkamata,” alisema Mashaka. Dudu Baya alipotafutwa na mwandishi wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa sero kwa saa sita kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Vero. “Vyumba vyake na vyangu haviingiliani kabisa, tumetenganishwa na ukuta hivyo shutuma zake hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi wa polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu baya

MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameswekwa rumande kwa kudaiwa kuchoma nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez Mabovu’, Mashaka Mrisho.

Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo mwenye nyumba sambamba na polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa madai ya kuchoma moto nyumba kwa makusudi na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
 

“Mkewe alitupia mkaa wa moto katika sofa, likashika moto kabla majirani hawajanisaidia kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha ndipo nikawapeleka polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja kumkamata,” alisema Mashaka.
 

Dudu Baya alipotafutwa na mwandishi wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa sero kwa saa sita kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Vero.


“Vyumba vyake na vyangu haviingiliani kabisa, tumetenganishwa na ukuta hivyo shutuma zake hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi wa polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu baya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni